Sasa unaweza kupata elimu sahihi ya Uislamu kwa wepesi na kwa gharama nafuu kabisa kwa kusoma Juzuu Saba (7) za Elimu ya Kiislamu kwa Posta (EKP).
Kwa wanafunzi wa Sekondari, hakuna tena sababu ya kuhofia kujiandikihsa kufanya mtihani wa Taifa wa Dini ya Kiislamu Kidato cha Nne. Hata kama hakuna walimu, jiunge na EKP.
Gharama za EKP ni:
 1. Kujiunga kwa kujaza fomu.
 2. Kununua Juzuu 7 kwa bei nafuu.
 3. Kusoma Juzuu na kufanya mitihani ya kila Juzuu.
 4. Kufanya mtihani wa kuhitimu baada ya kufaulu mitihani ya Juzuu 7.
 5. Kupata cheti cha kuhitimu (EKP) bure.

Katika juzuu hii kuna mada zifuatazo:

Mtazamo wa Uislamu juu ya Elimu

 • Maana ya Elimu.
 • Nani aliyeelimika.
 • Nafasi ya Elimu
 • Kwa nini elimu imepewa nafasi ya kwanza?
 • Chanzo cha elimu.
 • Dhana ya mgawanyo wa elimu.
 • Elimu yenye manufaa.

Mtazamo wa Uislamu Juu ya Dini.

 • Maana ya Dini
 • Kwanini mwanaadamu hawezi kuishi bila dini?
 • Aina kuu za Dini
 • Kwanini Uislamu ndio dini pekee iliyomstahiki binaadamu?

Imani ya Kiislamu.

 • Maana ya “Imani”
 • Nani “Muumini” wa Kiislamu?
 • Nguzo sita za Imani.
 • Maana ya kuamini kila nguzo ya Imani na athari yake katika utendaji wa maisha ya kila siku.

Lengo la kuumbwa mwanadamu hapa ulimwenguni.

 • Maana ya Ibada kwa mnasaba wa lengo la kuumbwa.
 • Mtazamo potofu juu ya Ibada.
 • Lengo la Ibada maalum

Hadhi na dhima ya Waumini katika Jamii.

 • Dhana ya khalifa
 • Nani watakaokuwa Makhalifa katika Jamii.
 • Dhima ya Waumini katika Jamii.

Juzuu hii inawasilisha mada zifuatazo:Shahada

 • Kutoa Shahada Mbili kiutendaji.
 • Maana ya Shahada ya Kwanza kiutendaji katika maisha ya kila siku
 • Maana ya Shahada ya Pili kiutendaji katika maisha ya kila siku.
 • Mwenendo wa Mtu aliyetoa Shahada mbili

Kusimamisha Swala

 • Umuhimu wa kusimamisha swala.
 • Lengo la kusimamisha swala
 • Maana ya swala.
 • Maana ya kusimamisha swala
 • Sharti za swala.
 • Nguzo na sunna za swala.
 • Namna ya kuswali kama kama alivyoswali Mtume(s.a.w)
 • Swala tano za faradhi katika nyakati za dharura.
 • Kusimamisha swala ya jamaa na Ijumaa
 • Swala za sunna
 • Tathmini ya swala zetu
 • Swala ya Maiti.

Zakat na Sadaqat

 • Maana ya zaka na swadaka
 • Umuhimu wa utoaji wa zaka na swadaqa
 • Masharti ya utoaji wa zakat na swadaqat
 • Mali inayojuzu kutolewa zakat,nisaab na kiwango cha zakat.
 • Lengo la utoaji wa zaka na swadaqa.
 • Tathmini ya utoaji wa zaka na swadaka katika jamii.

Swaumu

 • Maana ya Swaumu (Funga
 • Umuhimu wa Funga ya Ramadhani katika Uislamu
 • Kuonekana kwa mwezi wa Ramadhani
 • Nguzo za Funga
 • Yanayobatilisha Funga
 • Waislamu Wanaolazimika Kufunga Ramadhani
 • Sunnah na faradhi zinazoambatana na funga ya Ramadhani.
 • Funga za Kafara na funga za sunnah
 • Lengo la Funga
 • Funga inavyomuandaa mtu kuwa mcha-Mungu.
 • Tathmini ya ufikiwaji wa lengo la funga katika jamii.

Hija na Umra.

 • Maana ya Hijja na Umrah
 • Umuhimu na nafasi ya Ibada ya Hija katika Uislamu
 • Wanaowajibika kuhiji
 • Aina za Hijja
 • Matendo ya Hija na Umrah
 • Lengo la Hija na linavyofikiwa.
 • Tathmini ya Hija zetu.

 

Katika juzuu hii kuna mada zifuatazo:

Qur an

 • Uthibitisho kuwa Qur an ni kitabu cha Allah(sw)
 • Namna ya kuiendea Qur an
 • Mafunzo Maalum kutokana na sura/aya zilizochaguliwa
 • Mafunzo ya sura zilizochaguliwa katika juzuu Amma.

Sunna na Hadithi.

 • Maana ya sunna na hadithi
 • Nafasi ya sunna katika Uislamu.
 • Historia fupi ya uandishi wa Hadithi.
 • Uhakiki wa Hadithi sahihi
 • Tanzu na aina za Hadithi

Mwenendo wa Muislamu katika masaa 24.

 • Kuleta adhkar mbalimbali.

Katika juzuu hii kutakuwa na mada zifuatazo;

Ndoa ya Kiislamu

 • Maana na umuhimu wa ndoa
 • Kuchagua mchumba
 • Mahari
 • Kufunga Ndoa ya Kiislamu
 • Hekima na ruhusa ya kuoa wake wawili hadi wanne.

Wajibu katika familia

 • Wajibu wa mume kwa mke na mke kwa mume.
 • Wajibu wa wazazi kwa watoto na watoto kwa wazazi.
 • Wajibu kwa watumishi wa majumbani.
 • Wajibu wa majirani, mayatima na wasiojiweza

Talaka na Eda.

 • Maana ya talaka na eda
 • Mtazamo wa uislamu juu ya Talaka
 • Sulhu kati ya mume na mke.
 • Aina za talaka
 • Taratibu za kutaliki kiislamu.
 • Eda ya kuachwa na kufiwa na hekima yake.

Mirathi katika Uislamu

 • Maana ya Mirathi.
 • Wanaostahiki kurithi.
 • Mambo ya kuzingatia kabla ya Mirathi.
 • Ugawaji wa mirathi kwa kuzingatia Qur an (4:11,12 na 176)
 • Qur an inavyogawa mirathi.
 • Ugawaji wa mirathi.

Kudhibiti uzazi

 • Historia ya kampeni ya kudhibiti uzazi
 • Udhaifu wa hoja za makarifi juu ya kudhibiti uzazi.
 • Msimamo wa Uislamu juu ya kudhibiti uzazi

Hadhi na Haki za mwanamke katika jamii.

 • Hadhi na Haki za mwanamke katika jamii ya Kiislamu.
 • Hadhi na Haki za mwanamke katika jamii za kijahili.
 • Mtazamo wa Uislamu juu ya usawa kati ya mwanaume na mwanamke.
 • Hifadhi ya mwanamke na maadili ya jamii.

 

Juzuu hii inawasilisha mada zifuatazo;

Misingi ya Maadili

 • Maana ya Maadili.
 • Mtizamo wa Makafiri juu ya misingi ya Uadilifu
 • Mtizamo wa Uislamu juu ya misingi ya Uadilifu

Utamaduni

 • Maana ya utamaduni.
 • Ni upi utamaduni wa Muislamu?
 • Vipengele vya Utamaduni wa Kiislamu.

Sheria katika Uislamu

 • Maana ya sharia.
 • Umuhimu wa sharia katika jamii.
 • Chimbuko la sharia ya kiislamu.
 • Mgawanyo wa makosa katika sharia ya Kiislamu.
 • Haki za wasiokuwa Waislamu (Dhimmi)

Uchumi katika Uislamu.

 • Maana ya Uchumi.
 • Mfumo wa uchumi wa Kiislamu
 • Dhana juu ya uchumi kwa mtazamo wa Kiislamu.
 • Mazingatio muhimu katika uchumi wa Kiislamu
 • Wajibu wa serikali ya Kiislamu katika kusimamia uchumi
 • Haki na Uhuru wa kuchuma katika Uislamu
 • Biashara kwa mtazamo wa Uislamu.
 • Umuhimu wa benki katika uchumi.
 • Benki za Kiislamu.

Dola katika Uislamu

 • Maana ya Siasa
 • Maana ya Dola
 • Muundo wa Dola za Kitwaghuti na uendeshaji wake.
 • Muundo wa Dola ya Kiislamu na uendeshaji wake.
 • Sifa na wajibu wa kiongozi katika dola ya Kiislamu
 • Dhana ya Demokrasia katika dola ya Kiislamu
 • Usimamishaji wa Haki katika Dola ya Kiislamu.
 • Mifumo ya siasa

 

Katika juzuu hii kuna mada zifuatazo:

 • Dhana juu ya Historia.
 • Historia ya kuhuisha uislamu kabla ya Mtume (s.a.w)
 • Historia ya kuhuisha Uislamu wakati wa Mtume (s.a.w)
 • Uongozi wa Dola ya Kiislamu wakati wa Makhalifa wa Mtume (s.a.w)
 • Kuhuisha Uislamu wakati wa Tabiin.
 • Kuhuisha Uislamu katika karne ya 20 A.D
 • Harakati za kuhuisha Uislamu Tanzania.

Katika juzuu hii kuna mada zifuatazo:

 • Haja ya kuendeleza Uislamu katika jamii
 • Kuandaliwa Mtume Muhammad(s.a.w)
 • Maandalizi ya Mwanaharakati wa Kiislamu
 • Maandalizi ya Kundi la Harakati
 • Mbinu za Kulingania na Kusimamisha Uislamu katika Jamii
 • Mipango katika Harakati za Kiislamu
 • Uongozi bora katika Harakati za Kiislamu
 • Mwongozo wa Kujifunza na Kuujua Uislamu kwa Wepesi
 • Mbinu za Kufundisha kwa lengo la Kumuandaa Khalifa
PATA NAKALA YA JUZUU SABA, VITABU VYA ELIMU YA DINI YA KIISLAMU PAMOJA NA KIARABU KWA WARATIBU WA EKP KATIKA MIKOA YOTE TANZANIA BARA NA VISIWANI