Screen Shot 2020-10-05 at 6.03.39 PM

Utangulizi

Elimu ya Kiislamu kwa Posta (EKP) ni mfumo wa kujifunza kwa kutumia njia ya Posta kama sehemu ya mawasiliano baina ya Mwalimu na Mwanafunzi. kwa sasa EKP inaratibiwa kila Mkoa hapa nchini kwa kutumia Waratibu wa Elimu wa Mikoa.

 

Historia fupi ya Elimu ya Kiislamu kwa Posta (EKP) Tanzania

EKP ilianzishwa na Vijana wa Warsha ya Waandishi wa Kiislamu (WARSHA) mnamo mwaka 1983, ilipoanzishwa Shule ya Kiislamu ya Sekondari (Masjid Qubah and Islamic Centre). Tarehe 15 Julai 1985, Taasisi ya Islamic Propagation Centre (IPC) ilisajiliwa na kuchukua jukumu la kundesha EKP.

Mwaka 1986, IPC na MSAUD (Umoja wa Wanafunzi wa Kiislamu wa Chuo Kikuu Dar es Salaam) walikubaliana kushirikiana katika kuendesha Program hii ya EKP chini ya Mwalimu Mratibu. Mnamo Mei 1988, kutokana na mazingira ya Kisiasa na Kiusalama, Shura ya IPC na MSAUD iliamua kulirejesha jukumu la uendeshaji wa EKP kwa IPC.

Malengo Makuu ya EKP ni;

  1. Kuwawezesha wasomaji kuujua Uislamu kwa wepesi na kuutekeleza vilivyo
  2. kuandaa Walimu wa kufundisha “Elimu ya Dini ya Kiislamu (EDK)” katika Shule za Msingi na Sekondari
  3. kuwandaa walimu wa kufundisha Madrasa za Watoto na Watu Wazima
  4. kuwaanda Wanafunzi wa Sekondari kwa mitihani ya taifa ya Kidato cha pili na cha nne kwa somo la EDK

Tunamshukuru Allah(S.W) kuwa kozi ya EKP kwa kiasi fulani imewezesha wahitimu wake kufikia baadhi ya malengo hayo.

Wito

Wito wetu kwa waislamu ni kuwa kila Muislamu ajiunge na EKP, kisha awahamasishe watu wa Familia yake, Ndugu, Jamaa na Rafiki zake wa karibu na wao wajiunge na EKP. Ni tumaini letu kuwa Waislamu watakapo itikia wito huu wa kuijua na kuitekeleza Dini yao vilivyo, wataweza kuwa Makhalifa wa Allah (S.W) katika Jamii.

Tumuombe Allah (S.W) atuwafikishe katika hili.

Sasa unaweza kupata elimu sahihi ya Uislamu kwa wepesi na kwa gharama nafuu kabisa kwa kusoma Juzuu Saba (7) za Elimu ya Kiislamu kwa Posta (EKP).
Kwa wanafunzi wa Sekondari, hakuna tena sababu ya kuhofia kujiandikihsa kufanya mtihani wa Taifa wa Dini ya Kiislamu Kidato cha Nne. Hata kama hakuna walimu, jiunge na EKP.
Gharama za EKP ni:
  1. Kujiunga kwa kujaza fomu.
  2. Kununua Juzuu 7 kwa bei nafuu.
  3. Kusoma Juzuu na kufanya mitihani ya kila Juzuu.
  4. Kufanya mtihani wa kuhitimu baada ya kufaulu mitihani ya Juzuu 7.
  5. Kupata cheti cha kuhitimu (EKP) bure.
PATA NAKALA YA JUZUU SABA, VITABU VYA ELIMU YA DINI YA KIISLAMU PAMOJA NA KIARABU KWA WARATIBU WA EKP KATIKA MIKOA YOTE TANZANIA BARA NA VISIWANI